Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimewataka baadhi ya
viongozi wa Dini na Siasa wanaojaribu kushinikiza au kusuluhisha kundi
la umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kurudi bungeni kuendelea na mjadala
wa katiba mpya kutambua kwanza sababu zilizowatoa Ukawa ndani ya bunge
hilo na kwamba kundi hilo lipo tayari kurudi bungeni kama watakubaliana
kujadili rasimu inayotokana na maoni ya wananchi.
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa Singida
mashariki Mheshimiwa Tundu Lisu amesema hayo wakati akiwahutubia wakazi
wa mji wa Iringa katika viwanja vya soko la kihesa ambapo amesema umoja
huo hautakuwa na pingamizi lolote kuhusu kurudi kuendelea na mjadala wa
katiba mpya kama tu watakubaliana kujadili rasimu ya katiba hiyo
iliyowasilishwa na tume ya Jaji Joseph Warioba rasimu iliyotokana na
maoni ya wananchi.
Aidha Tundu Lisu ameongeza kuwa baada ya vyama vya upinzani kuunda
umoja wa katiba ya wanchi (UKAWA) kumezuka maneno mengi ya plopaganda
kutoka chama tawala yanayojaribu kuwakatisha tamaa wananchi akifafanua
kuwa plopaganda hizo ni hofu ya chama cha mapinduzi kuuogopa muungano
huo wa wapinzani.
Kwa upande wake mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
amewataka wananchi wa jimbo la iringa mjini kutotishwa na maneno ya
wapinzani wake kutoka chama cha mapinduzi wanaojaribu kuteka ajenda za
chadema jimboni humo kwa kisingizio cha utekelezaji wa ilani ya chama
tawala na kwamba yeye hatachoka kupigania maendeleo ya jimbo hilo na
wananchi wake.
0 comments:
Chapisha Maoni