Jumatatu, Juni 16, 2014

ETO'O KUKOSA MECHI DHIDI YA CROATIA

Nahodha wa Cameroon, Samuel Eto'o ana uwezekano mkubwa wa kukosa mechi ya Jumatano dhidi ya Croatia kutokana na jeraha la goti. Eto'o hajaweza kufanya mazoezi kwa siku mbili na huenda asiweze kupona. Eto'o ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter: 
Madaktari wamethibitisha kuwa huenda nisiweze kucheza kwa sababu ya jeraha la goti linalonipa maumivu.
Cameroon na Croatia zote zilipoteza mechi zao za ufunguzi.

0 comments:

Chapisha Maoni