HII ni kali lakini haikuwahi kuandikwa, staa wa Bongo Fleva, Ally
Timbulo alinusurika kuuawa baada ya kubainika kuwa anatembea na mke wa
mtu na mumewe kumsaka kwa udi na uvumba akiwa na bastola mkononi.
Akitema
cheche na Untold, Timbulo alisema, katika maisha yake hakuwahi
kufikiria kutoka kimapenzi na mtu ambaye yupo kwenye ndoa, isipokuwa
mwanadada huyo ambaye anafanya kazi serikalini (jina kapuni) alionesha
upendo wa dhati kwake pamoja na kumgharamia kwa kila alichohitaji.
Hakuwahi kuniambia kama ni mke wa mtu maana nilionana naye muda wowote nilipomuhitaji pia aliniganda vibaya mno na alikuwa tayari nimuoe, kumbe mumewe alikuwa ameshapata taarifa kuwa najiachia na mkewe, akanitafuta kwa njia ya simu na kunionya kuwa nikiendelea ataniua kwa bastola
alisema Timbulo.
0 comments:
Chapisha Maoni