Jumatano, Juni 11, 2014

MSIBA WA GEORGE TYSON WAZUA MAKUBWA KENYA, UKO MOCHWARI MPAKA SASA NI SUKU YA 14, NDUGU WAENDELEA NA SHUGHULI ZAO

KAMA huna taarifa, habarika sasa kwamba, mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ (41) aliyefariki dunia Mei 30, mwaka huu kwa ajali mbaya ya gari nchini Tanzania na kusafirishwa kwao,Kenya bado haujazikwa huku mazito yakiibuka kuhusiana na msiba huo!Chanzo cha ndani kimesema kwamba, mwili huo utazikwa keshokutwa Jumamosi kijijini kwao huko Kisumu baada ya kukaa mochwari kwa siku kumi na nne tangu kifo.
Katika hali ya kushangaza, utamaduni wa Kenya si kama wa Bongo, misiba hupewa kipaumbele siku za mwishoni mwa wiki, hasa Jumamosi.

Kwa sasa mwili upo mochwari, unasubiri kuzikwa Juni 14 (mwaka huu). Kwa hiyo ukifika kwenye nyumba yenye msiba ambayo ipo Donholm, Phase 5 jijini Nairobi, unaweza kusema hakuna msiba.
Watu wanaendelea na shughuli zao za kila siku, kama kwenda sokoni na sehemu nyinginezo.
Kifupi huwezi kujua kama kuna msiba. Huu ndiyo utaratibu wetu hapa Kenya, si kama huko Tanzania,

Ila Ijumaa ijayo, ndiyo kidogo kutaonesha kama kuna msiba kwani mwili utachukuliwa kwa ajili ya taratibu za kuaga kisha Jumamosi utapelekwa Kisumu, kwenye Kijiji cha Siaya ambako marehemu atazikwa.

0 comments:

Chapisha Maoni