Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku amekataa kwenda West Ham kwa mwaka
wa pili sasa, lakini huenda akajiunga na Wolfsburg ya Ujerumani (Daily
Mirror), Manchester United sasa wamemgeukia kiungo wa Bayern Munich,
Bastian Schweinsteiger baada ya kushindwa kumpata Thomas Muller (Daily
Star), Arsenal wapo tayari kutoa pauni milioni 5 kwa kipa Pepe Reina
(Metro), Arsenal pia wanataka kumsajili beki Bressan kutoka Gremio ya
Brazil (Daily Express), Arsene Wenger
pia anakaribia kukamilisha usajili wa Carlos Vela kutoka Real Sociedad
(Sun), Liverpool wana imani wataweza kumsajili Max Meyer kutoka Schalke
na kuwapiku Arsenal na Chelsea (Daily Express), kiungo wa Barcelona,
Alex Song ameambiwa yuko huru kuondoka Nou Camp, huku Manchester United
wakimfuatilia mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal (Talksport), rais wa
Real Madrid Florentino Perez ameruhusu klabu yake kumfuatilia Ramires wa
Chelsea (Marca), Paris St-Germain itamfuatilia kipa Petr Cech iwapo
Chelsea hawatamhitaji (Le Figaro), Atlètico Madrid wanafikiria kutoa
pauni milioni 18 kumsajili kiungo wa Arsenal Santi Cazorla (As.com).
0 comments:
Chapisha Maoni