Ijumaa, Juni 13, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 93 iliyopita, inayosadifiana na 13 Juni 1921 katika miaka ya mwanzo ya usimamizi wa Uingereza huko Palestina, kulianzishwa harakati kubwa katika ardhi yote ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na maghasibu wa Kizayuni. Harakati hiyo ilikuwa dhidi ya Wazayuni. Harakati ya wananchi hao ilibainisha upinzani wao dhidi ya siasa za kikoloni za Uingereza pamoja na uungaji mkono wa nchi hiyo kwa Wazayuni waliokuwa wameiteka ardhi ya Palestina. Siasa za Kikoloni za Uingereza zilijumuisha kuwashajiisha Wazayuni kutoka sehemu zote duniani waelekee Palestina ili kwa mujibu wa Azimio la Balfour, serikali ya Kizayuni iundwe ndani ya ardhi ya Palestina. Sera hiyo ya kikoloni ilitekelezwa mwaka 1948 wakati dola bandia la Israel lilipoundwa.

0 comments:

Chapisha Maoni