Ijumaa, Juni 13, 2014

ANDREA PIRLO KUSTAAFU SOKA BAADA YA KOMBE LA DUNIA

Kiungo mahiri wa kupiga pasi za mwisho wa timu ya taifa ya Italia Andrea Pirlo, amethibitisha kua atatundika daruga kuichezea timu yake ya Taifa mara maada ya mashindano ya kombe la dunia huko nchini Brazil yanayotarajiwa kuanza muda mchache kutoka sasa usiku huu.
Kiungo huyo wa Juventus Turin, ataelekeza nguvu zake kuitumikia klabu hiyo mabigwa wapya wa ligi kuu ya Italia Serie A, hii ikiwa ni baada ya kuongeza mkataba wake na mabingwa hao kwa miaka miwili zaidi.
Pirlo, 35, ameshacheza mechi 109 za Azzurri (timu ya taifa ya Italia), akiwa amewasaidia kunyanyua kombe la dunia mnamo mwaka 2006 walipoifunga Ufaransa kwa penati katika mechi ya fainali.
Pirlo alisema:
Nadhani ntastahafu baada ya Kombe la dunia, umri wangu ushaenda sasa, haupungui na kuwa mdogo, isitoshe, inabidi kuwapa fursa vijana wadogo wanaochipukia. Haitaleta maana kuendelea kuchezea timu ya taifa
Alimalizia maestro huyo.
Maestro Pirlo anatarajiwa kua moyo wa safu ya kiungo katika dimba la timu ya Italia katika mechi ya kwanza ya mashindano hayo dhidi ya Uingereza kundi D siku ya Jumamosi jioni.

0 comments:

Chapisha Maoni