Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa
kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil
kutazama michuano ya kombe la dunia
Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu
hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na
moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya usafiri kwenda Brazil.
Mmoja wa wachezaji hao alifurahi
sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao.
Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano, malazi na
usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama.
Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka
kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni
waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya
michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.
Hatua ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi
sana nchini Kenya kwa kuwa timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu
kushiriki michuano hiyo, sasa wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si
haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa
ajili ya usimamizi huo mbaya.
Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa
Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa kima cha dola elfu
arobaini. Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake hasa ni kuwapa
matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa.
Kenyatta mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil.
Ufadhili huu unakuja miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo.
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la
dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho
huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka
2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho
tarehe 18 Julai.
0 comments:
Chapisha Maoni