Ijumaa, Juni 13, 2014

HATIMAYE BACARY SAGNA NI MALI YA MANCHESTER CITY KWA MIAKA MITATU, NI BAADA YA KUSAINI MKATABA

Manchester City wamefikia makubaliano kumsajili Bacary Sagna kutoka Arsenal kwa mkataba wa miaka mitatu.
Beki huyo wa kushoto wa Ufaransa amekaa Emirates kwa miaka saba kabla ya mkataba wake kuisha mwisho wa msimu.
Sagna atakuwa akivaa jezi namba 3 kama aliyokuwa akivaa Arsenal, ambayo ilikuwa ikivaliwa na Maicon.
Arsene Wenger alimnunua Sagna kwa pauni milioni 7 kutoka Auxerre mwaka 2007.

0 comments:

Chapisha Maoni