Siku kama ya leo miaka 51 iliyopita sawa na tarehe 16 Juni 1963, Valentina Tereshkova mwanamke wa kwanza duniani kwenda angani kutoka Russia alianza safari yake ya angani kwa kutumia safina ya anga iliyoitwa Vostok-6. Mwanake huyo alitua katika orbiti ya ardhi wakati ambapo Valery Bykovsky mwanaanga mwingine wa Russia alipokuwa akizunguka mzunguko wa dunia. Valentina Tereshkova ambaye alielekea angani miaka miwili baada ya Yuri Gagarin mwanaume wa kwanza kwenda angani, alizunguka sayari ya dunia mara 48 kwa muda wa masaa 70 na dakika hamsini.
Na miaka 70 iliyopita katika siku kama ya leo inayosadifiana na tarehe 16 Juni mwaka 1944 ikiwa ni wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, wanajeshi wa majini wa Marekani waliaza kushambulia miji ya Japan kwa kuulenga mji wa Fokula ulioko kusini mwa nchi hiyo kwa mabomu. Mashambulizi hayo yalipelekea kuuawa makumi ya maelfu ya raia wa Japan na kuharibiwa viwanda na mashamba ya nchi hiyo. Vita hivyo vilipelekea Marekani kushambulia kwa mabomu ya nyuklia miji miwili ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki mwezi Oktoba mwaka 1945.
0 comments:
Chapisha Maoni