Alhamisi, Juni 12, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 100 iliyopita inayosadifiana na tarehe 12 Juni 1914, kwa mara ya kwanza kabisa yalifanyika majaribio ya kutumia nishati ya joto la jua pambizoni mwa Cairo mji mkuu wa Misri. Mbunifu na mtekelezaji wa mpango huo, alikuwa mwanafizikia wa Kijerumani, ambaye aliweza kukusanya miale ya jua, na kufanikiwa kuwasha mashine ya mvuke yenye kutumia 'horse power' 50.

Siku kama ya leo miaka 474 iliyopita inayosadifiana na tarehe 12 Juni 1540, Uhispania iliikalia kwa mabavu ardhi ya Chile iliyoko magharibi mwa Latini Amerika. Kabla ya hapo, Wahindi Wekundu wa Chile walizima shambulio la Uhispania iliyotaka kuivamia na kuidhibiti nchi hiyo. Mara baada ya Uhispania kuidhibiti Chile, mapambano ya Wahindi Wekundu yaliendelea katika kukabiliana na wakoloni hadi ulipofika mwaka 1817, ambapo Jose de San Martin Kamanda wa Kiajentina aliwashambulia wakoloni wa Kihispania huko Amerika ya Kusini, na kuandaliwa mazingira ya kujipatia uhuru nchi hiyo mwaka 1818.

Na siku kama ya leo miaka 796 iliyopita yaani mwaka 639 Hijria Qamaria alifariki dunia Ibn Yunus, faqihi mkubwa, tabibu na mwanahesabati. Alisoma masomo ya awali kwa baba yake na kustafidi na bahari ya elimu kwa wasomi wakubwa wa zama zake. Aidha Ibn Yunus alikuwa mtaalamu katika elimu na fani mbalimbali, ambapo alitokea kuwa mhadhiri na mwalimu katika shule kadhaa za mjini Cairo, Misri sambamba na kuandika vitabu vingi katika uwanja wa elimu ya dini na tiba. Mbali na kubobea katika elimu ya fiq'hi, Ibn Yunus alikuwa mtajika katika taaluma ya tiba, hesabu na elimu ya mziki.

0 comments:

Chapisha Maoni