Macho ya walimwengu na wapenzi wa soko dunia hii leo yanaelekezwa
nchini Brazil ambako masaa machache yamesalia hadi kuanza mashindano ya
Kombe la Dunia katika mchezo wa soka.
Mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo yanayozikutanisha timu za
mpira wa miguu kutoka nchi 32 duniani, itatanguliwa na hafla za ufunguzi
zitakazofanyika katika mji wa Sao Paul ambazo zinaenzi mazingira, watu
na mpira wa miguu.
Serikali ya Brazil inatumia jeshi la anga, askari polisi na wanajeshi
147,000 kuimarisha usalama huku shule za nchi hiyo zikifungwa wakati
huu wa mashindano hayo. Mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Kombe la
Dunia katika mchezo wa soka itafanyika katika uwanja wa Itaquerao kati
ya mwenyeji Brazil na Croatia.
Hayo yanajiri huku kukishuhudiwa migomo na malalamiko ya wananchi
ambapo Rais Dilma Rousseff wa Brazil ametetea uamuzi wa serikali yake wa
kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, na kutupilia mbali madai kwamba
wametumia gharama kubwa kuanda mashindano hayo. Ametangaza kuwa
matayarisho yamekamilika na kusisitiza kuwa uwekezaji katika ujenzi wa
viwanja vya mpira, viwanja vya ndege na miundombinu mingine utaipa nchi
hiyo faida za muda mrefu. Rais wa Brazil pia amewataka wananchi wa nchi
hiyo ya Amerika ya Latin kuunga mkono timu ya taifa hilo na kuwakirimu
wageni na watalii.
0 comments:
Chapisha Maoni