Mamlaka nchini Australia imetoa tahadhari dhidi ya matumizi ya
charger aina ya USB feki au zilizo chini ya viwango huku zikiwa
zimechomekwa kwenye umeme baada ya mwanamke mmoja kufariki dunia wakati
akitumia charger ya aina hiyo kucharge simu yake iliyokuwa imechomekwa
kwenye kompyuta yake ndogo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 alikutwa amevaa headphones
masikioni akiwa na kompyuta yake mikononi huku akiwa na majeraha ya
kuungua kifuani na masikioni nyumbani kwake huko Gosford, Kaskazini mwa
Sydney.
Polisi nchini humo bado wanafanya uchunguzi kujua mazingira ya kifo
hicho lakini kitengo cha biashara kilichofuatilia suala hilo
kimetahadharisha kuwa charger za simu zilizo chini ya viwango ni moja ya
sababu kubwa.
Mwanamke huyo ambaye ripoti zinadai kuwa anatokea nchini Ufilipino na
baadae kuwa raia wa Australia alivaa headphones zilizokuwa zimechomekwa
kwenye kompyuta ndogo iliyokuwa imechomekwa kwenye socket ya umeme.
0 comments:
Chapisha Maoni