Jumatatu, Juni 09, 2014

RONALDO DE LIMA UNAMKUMBUKA? HILI LINAWEZA KUMTOKEA KATIKA FIFA 2014 BRAZIL

Ronaldo de Lima, mchezaji wa zamani wa Brazil, huenda akapoteza rekodi yake ya kufunga magoli 15 katika michuano ya Kombe la Dunia.
Ronaldo alifunga bao lake la kwanza katika mechi dhidi ya Morocco mwaka 1998, ngazi ya makundi. Goli lake la mwisho na lililovunja rekodi alifunga mwaka 2006 dhidi ya Ghana.
Kwa kuwa Ronaldo amestaafu, rekodi yake sasa huenda ikachukuliwa na Miroslav Klose wa Ujerumani ambaye amefunga magoli 14 katika Kombe la Dunia.
Klose alifunga goli lake la kwanza katika Kombe la Dunia mwaka 2002 dhidi ya Saudi Arabia katika ngazi ya makundi.
Iwapo Klose atafunga angalau mabao mawili ataweka rekodi mpya.
Katika picha, Ronaldo de Lima alipotembelea jengo la utangazaji London Novemba 5 2013.

0 comments:

Chapisha Maoni