Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa
ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa
muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.
Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake.
Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya
utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa
pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC
kilishinda uchaguzi huo.
Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha
0 comments:
Chapisha Maoni