Jumatano, Juni 25, 2014

PIUS MSEKWA ADAI HAKUNA SABABU YA KUANDIKA KATIBA MPYA

Spika mstaafu, Pius Msekwa amesema haoni haja wala sababu ya msingi ya Tanzania kuandika Katiba Mpya kwa sasa kwani hakuna matukio makubwa ya kisiasa nchini yanayolazimisha kufanya hivyo.
Katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam jana, Msekwa alisema hata hivyo, anakubaliana na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuruhusu kufanyika kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu alikuwa na sababu zake na alikwishazieleza wazi.
Alisema,
Sioni haja ya kuwa na Katiba Mpya. Mnatunga Katiba Mpya kama kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa, yaani mabadiliko ya kiutawala
alisema.
Alifafanua Katiba ya Tanganyika na hata ya Tanzania ilibadilishwa pale palipokuwa na matukio makubwa ya kiutawala, lakini pia kuna matukio mengine ambayo hayakulazimisha kuandikwa upya kwa Katiba.

0 comments:

Chapisha Maoni