Chama cha Wananchi (CUF), kimefanya mabadiliko ya Katiba yake
ikiwa ni maandalizi ya kushirikiana na vyama vingine vinavyounda Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika uchaguzi ujao.
Katika mabadiliko hayo, chama hicho kinakusudia
kuingiza jimbo katika mfumo wake wa utawala ili uweze kufanana na wa
vyama vingine vya upinzani, hasa Chadema na NCCR-Mageuzi.
Hoja ya mabadiliko hayo iliwasilishwa jana katika
Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho unaoendelea Dar es Salaam ili
ijadiliwe na kupitishwa.
Akizungumza na wanahabari jana, Naibu Mkurugenzi
wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema hivi sasa Katiba ya chama hicho
inatambua kuwapo kata na wilaya lakini haitambui jimbo na kwamba
mabadiliko hayo ni maandalizi ya chama hicho katika kushirikiana na
Ukawa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu unaofuata.
0 comments:
Chapisha Maoni