Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana Sulley
Muntari na Kevin Prince Boateng wamefukuzwa katika timu hiyo kwa
ukosefu wa nidhamu.
Taarifa kutoka mtandao wa shirikisho la soka nchini humo imesema kuwa wawili hao wametimuliwa mara moja.
Boateng anayechezea kilabu ya
Schalke 04 amefukuzwa kwa kutoa matamshi machafu yaliomlenga mkufunzi wa
timu hiyo Kwesi Appiah wakati timu hiyo ilipokuwa katika mazoezi katika
eneo la Maceio.
Naye mchezaji wa AC Milan Sulley Muntari ameadhibiwa kwa kumshambulia afisa mmoja wa kamati kuu ya timu hiyo
Shirikisho la soka nchini Ghana limeongezea
kwamba kisa kinachomuhusu Muntari kilitokea siku ya jumanne na kumtaja
Moses Armah,mwanachama wa usimamizi wa timu hiyo kama mtu
aliyeshambuliwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.
Wakati huohuo Boateng amedaiwa kutojali matamshi
aliyoyatoa.Habari hizo zinajiri siku moja baada ya serikali ya Ghana
kutuma dola millioni 3 nchini Brazil ili kuwalipa wachezaji wa timu hiyo
nchini Brazil fedha zao za kushiriki katika michuano ya kombe la dunia.
Timu hiyo inayojulikana kama Black Stars ilikuwa
imetishia kususia mechi kati yake na Ureno iwapo haitapewa fedha hizo
swala lililoilazimu serikali kuingilia kati.
Ghana ina nafasi ya kufuzu katika michuano ya mchujo iwapo itaishinda Ureno na iwapo mshindi wa kundi G atakuwa Ujerumani.
0 comments:
Chapisha Maoni