Alhamisi, Juni 26, 2014

FAHAMU KUWA MAPENZI HAYAJI KWA BAHATI MBAYA

Si kweli kwamba, wapenzi wanapokutana kwa mara ya kwanza tu wanakuwa wamependana kwa dhati. Mapenzi hutengenezwa!
Hujengwa na hulindwa kwa muda mrefu. Kuna wakati ukifika, unaona hisia zako zinazidi kukua na kumpenda zaidi mwenzi wako. Si jambo la kushangaza ni matokeo ya wekezo la penzi kutoka kwa mwezi wako.
Hii inamaana kwamba, waliopendana kwa dhati leo, wakafunga ndoa kwa furaha mbele ya mashahidi, miaka mitano ijayo wanaweza kuchukiana kabisa.
Wanaweza kujuta ni kwa nini walioana. Hapo ni kwa sababu kuna mmoja wao au wote walishindwa kutengeneza mapenzi katika maisha yao halisi. Tengeneza upendo, onyesha hisia zako kwa mwenzako.
Acha kumuumiza mwenzako, wekeza zaidi na zaidi kwa mwenzi wako ili azidi kukupenda. Akikupenda zaidi nawe utampenda zaidi. Mtapendana zaidi na mtaishi maisha yenye furaha na amani zaidi.
Usiwaone leo wanapendana hata baada ya miaka 20 ya ndoa yao – waliwekeza upendo. Usihangae leo wanafarakana wakati juzi walikuwa pamoja kwa amani na upendo, kuna mmoja wao ameharibu upendo. Amechafua moyo wa mwenzake, hapo sababu ya kupendana inaondoka. – Joseph Shaluwa.

0 comments:

Chapisha Maoni