KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina
lake wala kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali
juu kwa kumuua mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara ya
kwenda Kawe-Beach.
Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo
iliwashtua na kuamua kusogea karibu ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye
jinsi ya kike akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na
puani.
0 comments:
Chapisha Maoni