Shirika moja la misaada limeitaka Facebook kurudisha
fedha ilizopata kwa kufanya matangazo ya kampeni yake rais Bashar
al-Assad wa Syria.
Matangazo hayo- ambayo sasa yametolewa na
Facebook- yalianzishwa mwezi Mei , na yamehusishwa na ukurasa unaoitwa
Sawa al-Assad. Sawa ina maana ya “pamoja”, neno ambalo alitumia rais
huyo kama kauli mbiu wakati wa kampeni.
Ukurasa huo ungalipo.
Utata umetokana na matangazo mengi yanayoendelea
kuukuza katika mtandao wa Facebook. Kwa kuwa matangazo haya yalikuwa
yamelipiwa, kampuni hiyo basi ilipokea fedha kwa matangazo hayo
yaliyoimarisha kampeni ya siasa zake Assad- jambo ambalo limelikera
shirika la kutoa msaada liitwalo ‘the Syria Compaign’.
Shirika hilo limetengeneza wavuti unaoitwa 'AdsForDictators.org unaokejeli Facebook' na unatoa malalamishi kwenye mtandao.
Wanafanya pesa mbovu kuwa nzuri
John Jackson
ambaye ni mkurugenzi wa shirika hilo aliiambia BBC.
Wanapaswa kutoa pesa hizo kwa shirika la misaada lenye sifa ambalo linawashughulikia wakimbizi wa Syria.
Haijulikani ni pesa ngapi, ingawa katika muda
mfupi ambao tangazo hilo lilifanywa, kuna uwezekano kuwa ni kiwango
kikubwa cha pesa.
Facebook bado haijasema chochote kuhusiana na
jambo hilo, ila tu kusema kwamba tangazo hilo halikufanywa kutoka Syria-
jambo ambalo litavunja masharti yaliyowekewa taifa hilo- na kwamba
kama kawaida sisi huondoa matangazo yasiyofuata kanuni zetu.
Hata hivyo, haijulikani hasa ni kanuni zipi
walizokiuka. Hakuna kabila lililotumiwa ambalo lina uchochezi, na pia
matangazo ya kisiasa katika mtandao wa Facebook hukubaliwa.
Itakumbukwa kuwa kampuni hiyo ilikuwa
imeorodhesha mbinu za kuwasaidia waliokuwa wakigombea nyadhifa
mbalimbali mwaka wa 2012 nchini Marekani kupitia kwenye Facebook.
0 comments:
Chapisha Maoni