Ijumaa, Juni 06, 2014

KIONGOZI WA WAISLAMU AMEFARIKI DUNIA NIGERIA

http://informationng.com/wp-content/uploads/2013/06/2013-06-17T010842Z_566800572_GM1E96H0KZM01_RTRMADP_3_NIGERIA.jpgKiongozi wa waisilamu katika jimbo la Kano nchini Ngeria,Al-Haji Ado Bayero, amefariki.

Kiongozi huyo mwenye kuheshimiwa sana miongoni mwa viongozi wengine wote nchini humo , amethibitishwa kufariki nchini humo.
Al-Haji Ado Bayero, alikuwa mtawala wa Kano tangu mwaka 1963 na alifariki baada ya kuugua kwa mda mrefu.
Tangu wakati huo Nigeria imekabiliana na misukosuko ya mapinduzi ya kijeshi na ghasia zingine.
Alikuwa na umri wa miaka 84 na kutambuliwa kama kiongozi wa muda mrefu sana na mkongwe zaidi wa waisilamu katika jimbo hilo na pia alitambulika kama kiongozi wa pili mwenye ushaiwishi zaidi kwa waisilamu Nigeria, Marehemu Emir pia alitambuliwa kama kiongozi aliyependa amani.
Miaka miwili iliyopita alinusurika kwa tundu la sindano baada ya msafara wake kushambuliwa ambapo dereva wake na walinzi wake wawili walifariki.
Ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali, Boko Haram, ndio waliomshambulia.
Boko Haram wamewashutumu viongozi wa kijadi nchini Nigeria kwa kuwa vibaraka wa wanasiasa. Juma lililopita Emir wa Gwoza aliuliwa na kundi hilo ambalo limetekeleza mashambulizi mengi Kaskazini Mashariki mwa nnchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Sa'ad Abdullahi mjini Abuja anasema kuwa emiralikuwa amerejea tu kutoka mjini London ambako alikuwa anapokea matibabu.

0 comments:

Chapisha Maoni