Bunge la jimbo la jiji la Nairobi nchini Kenya limepiga kura kuwaondoa makahaba katikati mwa mji mkuu.
Waakilishi katika bunge hilo walilazimika kupiga
kura mara tatu ili kufikia matokeo hayo. Kwa mara mbili matokeo ya kura
yalikuwa sare, lakini baada ya awamu ya tatu kura ya ndio ikashinda.
Hoja hiyo iliwasilishwa na
mwakilishi Bi Jane Mwasia, ikitaka wakuu wa jimbo kuwaondoa makahaba
mara moja kutoka katikati kwa jiji la Nairobi.
Waakilishi wanaume walipinga hoja hiyo mara tu
ilipowasilishwa lakini mjadala ulipotokota, wengi waliamua kupiga kura
ya ndio wakati wengine wakijizuia.
Mjadala huo nusura uzue makonde bungeni na kusababisha hisia mseto miongoni mwa waakilishi hao.
Baadhi ya waakilishi hao walipendekeza kuwa
sehemu maalum itengewe makahaba hao baada ya wao kundolewa katika
barabara zilizo katikati mwa jiji.
alisema mmoja wa waakilishi hao.
Mwakilishi mwingine, Manoah Mboko alisema kuwa
suluhu kwa makahaba sio kuwaondoa mjini bali ni kuwaoa kwani sheria ya
kuoa zaidi ya mke mmoja ilipitishwa maajuzi. Aliongeza kwamba makahaba
wanachangia pakubwa sana katika uchumi wa mji wa Nairobi.
Mwakilishi mwingine alizua kicheko aliposema kuwa dunia nzima ni kama soko na hivyo kila mtu aruhusiwe kuuuza bidhaa zake.
0 comments:
Chapisha Maoni