Ijumaa, Juni 06, 2014

CHRIS BROWN AWA BONGE BAADA YA KUTOKA JELA

Picha za kwanza tokea Chris Brown atoke Jela zimetoka na kama wengi mlivyotegemea mtu akitoka jela za bongo anakua amekonda basi jiulize tena coz jamaa katoka jela huku akiwa ameongezeka unene hadi mtu unaweza kumuita kibonge. Birthday yake ya kusherekea miaka 25 ilikua tarehe 5 mwezi wa tano lakini sababu alikua yupo jela wakaamua kuiunganisha na sherehe ya kukaribishwa nyumbani.
Huku akiwa amevalia nguo za kijeshi ambazo kibongobongo lazima wakukamate ni wazi Chris alikua ameongezeka uzito lakini akiwa mwenye afya nzuri. Inaelekea maisha ya jela yalikua mazuri sana kwa Chris.Kilichobaki kwa chris sasa ni kutoa ring yake puani na kuanza kuachia ngoma kali.
Chris Brown aliachiwa tarehe 2 mwezi wa 6 baada ya kukaa jela kwa siku 59. Kwenye Sherehe hiyo kulikua na mama yake, girlfriend wake Karrauche Tran, Tyga, T-Pain na bikini models wa kutosha.

0 comments:

Chapisha Maoni