Ijumaa, Juni 06, 2014

MO MUSIC APAGAWA DAR ES SALAAM

CHIPUKIZI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amesema ameshangazwa na mapokezi aliyoyapata Dar es Salaam na hakutarajia kuona mashabiki wengi kupagawa pindi anapokuwa stejini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Club Bilicanas wakati akiwa anatambulisha video ya ngoma yake ya ‘Past Member’, ambayo inafanya vizuri katika tasnia hiyo kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake.
Alisema, hakutegemea kama kwa muda mfupi alioingia katika tasnia hiyo anaweza kupata wadau wengi katika Jiji la Dar es Salaam, kwa sababu ndio ilikuwa shoo yake ya kwanza tangu alipoingia katika tasnia hiyo.
Mo alisema kuwa, atafanya kila mbinu kuwa tofauti na wasanii wenzake ili azidi kuwapagawisha mashabiki wake mbali na ilivyo sasa.
Aliwataka mashabiki wake, wakae tayari kuzidi kupokea vitu vizuri zaidi kutoka kwake na pia wasanii wenzake waweze kujipanga, kwani anajua yeye ni mkali.

0 comments:

Chapisha Maoni