Ijumaa, Juni 06, 2014

MPOKI KATIKA BIFU NA WAANDISHI WA HABARI...ADAI HAWANA AKILI

KATIKA hali isiyo ya kawaida mchekeshaji maarufu, Mujuni Sylivester ‘Mpoki,’ ametangaza rasmi mgogoro na waandishi wa habari kwa kutoongea nao kwa madai kwamba wengi wao hawana akili.
Bila ya kutaja sababu ya kufikia uamuzi huo hata pale alipooulizwa na safu hii, Mpoki alisema ameshajiapiza kutoongea nao, msimamo ambao anaamini atausimamaia katika maisha yake.
Wakati akiweka msimamo huo, tetesi zilizoifikia safu hii ni kwamba Mpoki ametangaza mgomo huo baada ya kukosolewa na vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii, kwa kuwatusi wasanii mbalimbali na waalikwa wengine wakati akiwa MC katika tukio  la Tuzo za Muziki za Kilimanjaro’KTMA 2014’ zilizofnyika usiku wa Mei 3 kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

0 comments:

Chapisha Maoni