Ijumaa, Juni 06, 2014

BATULI: KILA NIKITAKA KUREKODI FILAMU NAPANDWA NA MARUHANI (MASHETANI)

NYOTA wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, amesema kila aingiapo kwenye kazi ya kurekodi filamu, anapatwa na tatizo la kupandisha maruhani (mashetani), jambo ambalo linamkosesha raha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Batuli alisema kuwa hawezi kumhisi mtu yeyote vibaya juu ya tatizo hilo, lakini hali hiyo inamkosesha amani, kwani haelewi chanzo chake.
Mimi kwa kweli sitaki kabisa kuweka imani tofauti ya kumhisi mtu vibaya, ila najiuliza kwanini nipandishe maruhani wakati wa kurekodi peke yake?
alisema Batuli.
Batuli aliongeza kuwa kinachomchosha zaidi, hata akienda hospitali haonekani kama ana tatizo lolote, hali ambayo inampa mawazo zaidi.
Aliongeza kuwa hana jinsi ya kufanya, kilichobaki ni kumuomba Mungu aweze kumsaidia ili aweze kuepukana na hali hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni