Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya
kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo
wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa
usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na
kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa
ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi
ijayo.
Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana.
0 comments:
Chapisha Maoni