KAMISHNA wa Polisi Jamii nchini, Musa Ally Musa, amepiga marufuku
Polisi Jamii kutumia silaha za mapanga katika ulinzi badala yake
watumie filimbi.
Musa alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na
waandishi wa habari na kusema kutokana na changamoto iliyopo kwa jamii,
ya kutokuelewa maana ya Polisi Jamii kunachangia polisi hao kuonekana
kama majambazi.
Alisema Polisi Jamii wanapoona tukio la uhalifu wanatakiwa watumie
filimbi kwa kuwa wengi wao hawana sare wala vitambulisho, pia watoe
taarifa kwa askari kata ambaye yupo eneo la tukio ambaye ndiye mwenye
majukumu ya kutoa silaha.
Tangu kuanzishwa kwa Polisi Jamii mwaka 2006, imesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya uhalifu
alisema.
Alisema Polisi Jamii maana yake ni ushirikishwaji wa kila mtu aliyemo ndani ya Jamii kulingana na nafasi yake aliyokuwa nayo.
0 comments:
Chapisha Maoni