Jumanne, Juni 10, 2014

LEO KATIKA HISTORIA

Miaka 224 iliyopitaka katika siku kama ya leo inayosadifiana na tarehe 10 Juni 1790 vikosi vya jeshi la Uingereza viliivamia ardhi ya Maleya inayojulikana hii leo kama Malaysia. Wakati huo Uholanzi ilikuwa ikiikoloni Maleya na kupora utajiri mkubwa wa nchi hiyo wa madini ya bati. Kwa kuingia vikosi vya Uingereza Maleya iliibidi Uholanzi ianze kuondoka nchini humo na ilipofikia mwaka 1824 Uholanzi ilikubali kuiachia Uingereza ardhi hiyo kwa sharti kwamba nayo iachiwe Indonesia ambayo ilikuwa ina umuhimu mkubwa kwa Uholanzi. Malaysia ilijipatia uhuru wake mwaka 1957 na Indonesia mwaka 1956.

Siku kama ya leo miaka 14 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 10 Juni mwaka 2000, alifariki dunia Rais Hafidh Asad wa Syria baada ya kuugua kwa muda mrefu. Hafidh Asad alizaliwa mwaka 1930 na aliteuliwa kuwa kamanda wa vikosi vya anga vya Syria mwaka 1964, miaka mitatu baadaye alichaguliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo. Ilipofika mwaka 1970 kupitia mapinduzi ya kijeshi, Hafidh Asad alitwaa madaraka ya nchi hiyo na baadaye kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Baath. Miongoni mwa sifa za siasa za nje za Syria wakati wa urais wa Hafidh Asad, zilikuwa ni kutofanya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuimarisha uhusiano na nchi zinazopinga Uzayuni kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Na Siku kama ya leo miaka 937 iliyopita aliaga dunia Hassan bin Hafiz Ghassani mpokeaji hadithi na tabibu mashuhuri wa Andalusia, sehemu ya Uhispania ya leo. Ghassani alikuwa mwanafasihi mahiri na tabibu mweledi. Aidha alikuwa na hati za kuvutia sana na mwenye kipaji kikubwa cha kutunga mashairi.

0 comments:

Chapisha Maoni