Jumanne, Juni 10, 2014

FIFA 2014 BRAZIL...2 DAYS LEFT: IFAHAMU SIRI KUBWA ILIYOPO KATIKA NEMBO YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Kila Kombe la Dunia lina taswira yake ya kipekee. Tarswira hiyo huoneshwa kupitia nembo maalum. Nembo hiyo rasmi ya Kombe la Dunia huwakilisha michuano yenyewe na nchi inayoandaa michuano hiyo kwa dunia.
Nembo rasmi ya Kombe la Dunia Brazil 2014 inajulikana kama "Kuhamasisha". Nembo hiyo ina picha ya mikono mitatu inayounda mfano wa Kombe la Dunia. Mikono hiyo mitatu ina rangi za manjano na kijani. Rangi hizi zinatoa ishara kuwa Brazil inakaribisha Ulimwengu mzima nchini humo.
Nembo hiyo imechaguliwa na jopo la wataalam, ambao walipitia nembo nyingine zipatazo 25 zilizopendekezwa na taasisi mbalimbali nchini Brazil.

0 comments:

Chapisha Maoni