Arsenal huenda wakamkosa kipa wa Real Madrid,
Iker Casillas, baada ya mpenzi wake kudai kuwa hatohama kutoka mji mkuu
wa Spain, Madrid (Daily Express),lakini Arsenal huenda wakamsajili
mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro
Morata na wapo tayari kupambana na Tottenham na Inter Milan wanaomtaka
pia (Daily Express), Barcelona wamefikia makubaliano yasiyo rasmi na
Marcus Reus wa Borussia Dortmund. Reus amekuwa akifuatiliwa pia na
Manchester United (Talksport), wakati huohuo Manchester United wapo
tayari kupokea pauni milioni 12 kwa kiungo wake Marouanne Fellaini
ambaye alisaini mwaka jana kutoka Everton kwa pauni milioni 27 (Daily
Star), Chelsea wanajaribu kumsajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona
katika mkataba ambao utahakikisha Arsenal haipati nusu ya faida
itakayopata Barcelona (Daily Telegraph), Pepe Reina atarejea Liverpool
kwa kuwa Napoli inashindwa kufikia madai ya Liverpool ya kubadili
mkataba wa mkopo kuwa wa moja kwa moja (Metro), Manchester City
watakamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Porto, Fernando ifikapo
mwisho wa wiki hii na pia kukamilisha usajili wa Bacary Sagna kutoka
Arsenal(Daily Mail), Everton wana tumaini watafanikiwa kupambana na
Arsenal katika kumsajili Samuel Eto'o kutoka Chelsea (Daily Express).
Share tetesi hizi na wapenzi wa soka.
0 comments:
Chapisha Maoni