Jumanne, Juni 10, 2014

BAADA YA RAY C KUJIONA AMEPONA, AMVAA KHADIJA KOPA BILA WOGA

MWANADADA ambaye alitamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya miaka ya nyuma, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema ujio wake mpya kwenye muziki atakuja pia na taarabu huku akimtaka malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa, ajiandae kupambana naye.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Ray C, alisema kwenye albamu yake ambayo inakuja hivi karibuni, kuna mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali zikiwemo taarabu na za Kihindi.

Nimefanya taarabu kama mbili na zouk, yaani nimebadilika kabisa, kuna kwaito, Bongo fleva, kihindi kidogo na taarabu nimeimba pia, kwa hiyo Malkia Khadija Kopa ajiandae, kwani nakuja kuvamia tasnia hiyo
alisema.
Aliongeza kuwa muziki anaokuja nao sasa hivi ni ule wa kuonyesha kipaji cha kuimba na sio kucheza kama alivyokuwa zamani.
Ray C alishawahi kutamba na ngoma zake kama, ‘Milele Daima’, ‘Watanionaje’, ‘Uko Wapi’ na nyinginezo nyingi huku akinogesha na manjonjo ya kukata kiuno hadi kubatizwa jina la ‘Kiuno bila mfupa’.

0 comments:

Chapisha Maoni