Ijumaa, Juni 13, 2014

KUHUSU MADIWANI WALIOTAFUNA MAMILIONI MANISPAA YA ILALA

Kitendo cha Madiwani wa Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam kutafuna mamillioni ya Fedha za walipa Kodi kupitia mgongo wa ziara ya kifisadi kwamba walikwenda Mtwara kujifunza Kilimo cha zao la Muhogo, Kilimo ambacho kimsingi hakina tija wala suluhu ya matatizo Sugu yaliyodumu ndani ya manispaa hiyo kwa kipindi cha miaka zaidi ya hamsini ya Uhuru, ni kutowatendea haki Wananchi wa Jimbo la Ilala wanaotaka kuona Huduma bora ya Maji Safi na Salama, Elimu bora mashuleni, Afya na Miundombinu kama vile Barabara zilizochakaa na kubakia mashimo tupu.

0 comments:

Chapisha Maoni