Daniel Day-Lewis atapewa cheo cha Sir, na
Angelina Jolie atapewa cheo cha Dame kwa kampeni yake ya kupambana na
uhalifu wa ubakaji wa wanawake katika maeneo ya vita, pamoja na kazi
zake nyengine kwa niaba ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
wakimbizi, UNHCR.
Na waandishi wawili wa BBC wamepata nishani ya OBE:
Lyse Doucet, mwandishi mkuu wa BBC katika maswala ya kimataifa, na Tin Htar Swe, mhariri wa Idhaa ya BBC ya lugha ya Burma.
Stephen Sutton, kijana wa miaka 19 aliyekufa
karibuni kutokana na saratani, na wakati akiugua aliongoza mchango wa
karibu dola milioni 7 kugharimia utafiti dhidi ya ugonjwa huo, ametunzwa
MBE, (ambayo alipokea kabla ya kufariki mwezi uliopita.)
Mtunzi wa riwaya, Hilary Mantel, aliyeandika
vitabu vilivyopata zawadi ya Booker, 'Wolf Hall' na 'Bring up the
Bodies', piya amepewa hadhi ya Dame.
0 comments:
Chapisha Maoni