Jumatano, Juni 25, 2014

AMMY NANDO AELEZA HAJA YAKE YA KUMUOA LULU WA BONGO MOVIE

Ammy Nando na Lulu walitengeneza vichwa vya habari mara kadhaa wakihisiwa kuwa na uhusiano wa mapenzi. Hata hivyo wawili hao kwa nyakati tofauti waliueleza uhusiano wao kuwa ni wa kirafiki.
Lakini Nando bado anamuangalia Lulu kwa jicho la tatu kama wife material. Nando amefunguka yote katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr na DJ RGuy. Amesema Lulu ni rafiki yake, lakini ni msichana ambaye anamzimia kwa kuwa anajua kutafuta pesa japo ana umri mdogo.
Lulu ni mwanaharakati, ni mdogo lakini she knows how to get money.
Amesema Nando.
Aongeza kuwa kutokana na sifa alizonazo za kutafuta pesa pamoja na uzuri wake, atakapokuwa na mpango wa kuolewa yeye yuko tayari kutulia nae.
Kama Lulu akikubali kuolewa, me I settle down….nitatulia kwa Lulu kama akikubali kuolewa…..hata kwa muonekano ni mkali
Alisikika Nando
Hivi karibuni Lulu alisema kuwa hana uhusiano wa mapenzi na Nando na ana mpenzi wake mwingine.
Nando pia alieleza uhusiano wake na Dayna Nyange na kudai kuwa ni rafiki yake tu na wanashirikiana katika video ya wimbo wake mpya
nitauza sura mle ndani.
Baada ya kupata hayo maelezo kutoka kwa Nando, naomba nikwambie kitu kingine muhimu. 

0 comments:

Chapisha Maoni