Alhamisi, Juni 26, 2014

WANAFUNZI 100 WAUAWA KWA RISASI MAREKANI

Ripoti mpya imeonesha kuwa, watoto wasiopungua 100 wameuawa kwa kupigwa risasi bila kukusudia nchini Marekani, mwaka mmoja baada ya kutokea tukio la kushambuliwa wanafunzi katika shule ya msingi ya Newtown, huko Connecticut.
Ripoti hiyo ni ya hivi karibuni zaidi uliyochunguza madhara ya kutapakaa bunduki katika jamii.
Mkuu wa uchunguzi huo John Feinblatt, amesema kuwa mauaji hayo yanaweza kuzuilika, ingawa mara nyingi huwa wanasema kwamba yametokea bahati mbaya au hayakuweza kuzuilika. Uchunguzi huo umeonesha kuwa, katika asilimia 73 ya matukio hayo, mauaji yalisababishwa na mfyatuaji risasi mwenye umri mdogo wa miaka 14 au chini ya hapo.  Katika asilimia 57 ya matukio ya aina hii wahanga walipigwa risasi na mtu mwingine na katika asilimia 35 ya matukio, wahanga walijipiga risasi wenyewe.

0 comments:

Chapisha Maoni