Alhamisi, Mei 01, 2014

YOTE KUHUSU 'JB' WA BONGO MOVIE KUMILIKI CASSINO

Jacob Steven ‘JB’ amezua utata kwenye klabu mpya ya Princess Cassino iliyopo Posta mpya, Dar kufuatia minong’ono kuwa, yeye ndiye mmiliki wake.
Hali hiyo ilijitokeza juzi kati kwenye uzinduzi wa klabu hiyo ambapo msanii huyo ndiye alionekana kuwa mwenyeji kwa kukatiza kila mahali.

Hivi, JB ndiye mwenye hii klabu nini? Mbona kama mwenyeji kuliko wengine. Anakaribisha wateja, anafuatilia watu kama wanapata huduma sahihi
alisikika mteja mmoja.
JB alilpoulizwa juzi alikiri kuwa mmoja wa waratibu wa mambo ya burudani ya Cassino hiyo lakini si mmiliki.

0 comments:

Chapisha Maoni