Alhamisi, Mei 01, 2014

HUYU JAMAA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUSEMA 'RAIS AACHE BANGI'

Sio jambo la kawaida mtu kujiamini na kumtukana Rais wa nchi na taarifa hiyo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari lakini kwa Samuel Onkwami imekua rahisi kwake ila imemgharimu maana sasa hivi yuko kwenye sehemu atakayoshughulikiwa.
Ni mwakilishi wa Wadi ya Kiogoro Kaunti ya kisii huko Kenya na sasa amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kudai kwamba Rais Uhuru Kenyatta anavuta Bangi ambapo ishu ilianzia pale alipokaririwa Kanisani akihutubia na kusema ‘walio karibu na Rais Uhuru Kenyatta sharti wamshauri aache kuvuta Bangi’’
Kiongozi wa mashtaka ameiambia mahakama ya kisii kwamba mwakilishi huyo wa wadi alitoa matamshi hayo katika kijiji cha karera na sheria inayo mshtaki mtuhumiwa inasema ni hatia kwa yeyote kutoa matamshi kama hayo kuhusu mtumishi wa umma  .
Samuel ambae ni baba ya watoto watano anataaluma ya Teknolojia ya maabara kutoka chuo kikuu cha Teknolojia Mombasa na amewahi kuhudumu katika ofisi za hazina ya ustawishaji eneo Bunge kabla ya kuingia kwenye siasa mwaka wa 2007 na baadae kuchaguliwa mwaka uliopita kuwa mwakilishi wa Wadi.

Mawakili wa mshukiwa ambao ni Gideon Nyambati na Isaiah Mosota wameiomba mahakama hiyo kumuachia huru mshukiwa kwa dhamana na kuomba upande wa mashtaka kuwapa ushahidi na malalamishi dhidi ya mteja wao ili kujiandaa vyema kwa ajili ya kutoa utetezi wao.

0 comments:

Chapisha Maoni