VIONGOZI wa Yanga wakiongozwa na Seif Ahmed
‘Magari’, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya ziada kumbakiza beki wao,
Mbuyu Twite kutotua Azam.
Juhudi za kumbakiza Twite zilianza juzi usiku mara tu baada ya Azam
FC kufanya kufuru ya kumsajili kiungo Frank Domayo wa Yanga, siku mbili
tu baada ya kumnasa Didier Kavumbagu, lakini mpaka jana jioni Yanga
walikubali lolote liwe.
Kweli jana Yanga walikutana na Twite kwa kuwa walitaka wamalizane naye kuhusiana na suala hilo
kilieleza chanzo na kuendelea:
Unajua Twite kawaeleza kila kitu kwa kweli. Kweli Azam FC walimuita na kujadiliana naye kuhusiana na suala hilo, lakini kawatajia dau kubwa ambalo linaweza kuwashinda, mpaka mwisho wa kikao Twite kaambiwa achague dau dogo la Yanga au kubwa la Azam kwa kuwa wao (Yanga) wameona kiwango alichotaja ni cha juu mno.
Twite pia mkataba wake umekwisha, hivyo yupo huru na wao wanataka beki mzoefu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Hivyo Twite ni chaguo lao na ndiyo alikuwa mchezaji wa kwanza kabisa wanamtaka, sasa sijui ilikuwaje wakaanza na wengine!
Viongozi wa Yanga hawakutaka kulizungumzia hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni