Jumapili, Mei 25, 2014

WENJE AWASHA MOTO MWANZA, ADAI UKAWA HAWARUDI NG'O BUNGENI MPAKA WABEMBELEZWE

Mbunge wa Nyamagana kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ezekia Wenje, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya fedha ya Ukawa, anasema kuwa hawatarudi kwenye Bunge la Katiba kama njia za kistaarabu hazitatumika kuwaomba warudi.
Wenje alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza katika viwanja vya Dampo mkoani humo.
Akishangiliwa na umati huo wa watu, Wenje anasema Ukawa wataendelea kudai Katiba ya Wananchi hadi pale itakapopatikana. 
Kutokana na mapambano yangu bungeni sasa jina limebadilika. Najulikana Jenero na siyo mtoto wa mama ntilie tena na kwa kudhihirisha hilo nitahakikisha maoni ya wananchi hayachakachuliwi na Katiba itakayopatikana itakuwa ya wananchi wote
anasema.
Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) namtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda atumie njia za kistaarabu na kuonyesha ustaarabu katika kutusihi turudi kwenye Bunge Maalumu la Katiba mwezi Agosti la sivyo, hatutarejea ng’o
anasema

0 comments:

Chapisha Maoni