Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Saimoni Bolisha mwenye 22 na Maraku Thadesa raia wa kutoka nchini Ethiopia wanashikiliwa kwa tuhuma za kuingia nchini bila kuwa na kibali maalumu cha safari.
Aidha, ameongeza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa na askari polisi wakiwa doria Mei 20,Mwaka huu majira ya saa 10:00 asubuhi maeneo ya barabara mbili Kata ya Makorongoni Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.
Hata hivyo,Kamanda Mungi ametoa wito kwa jamii kushirikiana na jeshi la polisi ili kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa katika mamlaka husika pindi wanapomkuta mtu/watu wenye mashaka nao hasa raia wakigeni.

0 comments:
Chapisha Maoni