atu wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya tangu jana kwa kukutwa na nyara za serikali katika kijiji cha kisungu-mkwangu, kata ya mamba,tarafa ya kiwanja wilaya ya chunya mkoani Mbeya.
Katika tukio hilo, jeshi la polisi limewakamata Nayoramu Wajekaje [42] mkazi wa kijiji cha mkwangu na Majigita Mussa [40] mkazi wa Uvinza mkoani Kigoma baada ya kukamatwa wakiwa na nyara za serikali ikiwa ni pamoja na nyama ya mnyama Insha yenye uzito wa kilo 3 pamoja na ngozi ya kichwani ya mnyama huyo.
Aidha taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi zinaeleza kuwa watuhumiwa hao wawili ni wawindaji haramu na taratibu za kisheria zinafanywa ili kufikishwa mahakamani.
Pamoja na hayo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na uwindaji haramu kwani ni kinyume cha sheria, badala yake wafuate taratibu zilizopo kwa mujibu wa sheria za nchi.

0 comments:
Chapisha Maoni