Wakazi wa mkoa wa Iringa wamekumbushwa kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayotokea kwenye sehemu nyingi nchini.
Mtafiti wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a amesema wananchi wanapaswa kutunza uoto wa asili na mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi hususani wananchi wa kijiji cha Isimani kilichopo wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani ambacho kilikuwa kinaongoza kwa uzalishaji wa mazoa ya chakula ambapo kwa sasa kumekuwa uhaba wa chakula.

Dkt. Chang’a amesema, matumizi ya nishati za magari, gesi na vyombo vya usafiri zikiwemo ndege pamoja na ukataji wa miti ovyo umepeleka kutokea kwa mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye sehemu kubwa nchini.
Naye Diwani wa kata ya Kihorogota, tarafa ya Isimani wilayani Iringa Vijijini Bw. Costantino Kihwelo amesema, miti ya asili ikipandwa kwa wingi itasaidia kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Naye mwalimu wa shule ya sekondari ya Ebenezer amesema, msingi wa utunzaji wa mazingira unaanzia shuleni huku wanafunzi wakishauriwa kupanda miti na kuimwagilia.
Hata hivyo, Dkt. Chang’a ameshauri wakazi wa tarafa ya Isimani kupanda mazao yanayostahimili ukame ili kutunza vyanzo vya maji na kuthamini mazingira ili iwe lulu kwa vizazi vijavyo aidha amesema zoezi hilo linakwenda na kauli mbiu ya “panda miti kata mti”.

0 comments:
Chapisha Maoni