Mtu mmoja ameuawa dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali kwa kuhisiwa kuwa ni jambazi jana majira ya saa nane mchana, maeneo ya Ilemi Juhudi hapa jijini Mbeya.
Taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi mkoani Mbeya zimemtaja marehemu kwa jina la Kitwana Lugoya, 30, mkaazi wa Ilemio-Juhudi na kueleza kuwa alikumbwa na umauti baada kushambuliwa sehemu mbali mbali za mwili na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi kama vile mawe, fimbo na marungu.
Aidha kwa mujibu wa taarifa hizo ni kwamba chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za unyang’anyi au utekaji wa gari, inasemwa kuwa marehemu akiwa na wenzake watatu walifanya tukio la utekaji katika barabara ya mbalizi/mkwajuni katika kijiji cha mshangamwelu, kata ya mshewe, tarafa ya bonde la usongwe wilaya ya mbeya vijijini mkoa wa mbeya baada ya kuweka mawe barabarani na kisha kuteka gari aina ya fuso.
Katika tukio hilo, Stephen Mgogo [40] mkazi wa kabale akiwa na wenzake kwenye gari walishambuliwa kwa silaha za jadi mapanga na marungu kisha kuporwa pesa, simu za mkononi na pikipiki moja T.682 CHT aina ya SANYA iliyokuwa ndani ya gari hilo na kutoweka kusikojulikana. Thamani halisi ya mali iliyoporwa bado kujulikana.
Kufuatia msako uliofanywa na jeshi la polisi kumepelekea kupatikana kwa pikipiki pamoja na watuhumiwa wawili Ndayobi Lutego [26] mkazi wa igunga-tabora na Iddi Sadick [29] mkazi wa veta wakati Mhanga Stephen Mgogo amelazwa hospitali teule ya ifisi hali yake inaendelea vizuri.
Pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata watuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali badala yake wahakikishe wanawafikisha katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao ichukuliwe

0 comments:
Chapisha Maoni