Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo wameshindwa kuonesha utu ipasavyo kwa
msanii mwenzao, William Mtitu ambaye hivi karibuni alifiwa na baba yake
mzazi.
Baba wa msanii huyo, John Mtitu alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani na alipofanyiwa upasuaji, hakuweza kuzinduka.
Baba wa msanii huyo, John Mtitu alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani na alipofanyiwa upasuaji, hakuweza kuzinduka.
Katika hali ya kushangaza, wasanii waliofika nyumbani kwa msanii
huyo, Mburahati jijini Dar walionesha kususia baadhi ya vitu na
kuwafanya waombolezaji kuwashangaa.
Licha ya mara kadhaa wasanii hao
kutakiwa kwenda kuchukua chakula, wengi walionekana kujifanya kama
hawasikii huku wakiendelea kupiga stori zao.
Cha kushangaza zaidi, baada ya msosi kuisha, baadhi walienda kuagiza soda na keki kitendo kilichotafsiriwa kuwa, walikuwa na njaa lakini walifanya makusudi kususia chakula.
Cha kushangaza zaidi, baada ya msosi kuisha, baadhi walienda kuagiza soda na keki kitendo kilichotafsiriwa kuwa, walikuwa na njaa lakini walifanya makusudi kususia chakula.
Baada ya zoezi la chakula, mwili
uliingizwa nyumbani kwa dakika tano na baadaye ukapelekwa katika
Kanisani la Katoliki Parokia ya Mburahati kwa ajili ya ibada kabla
kusafirishwa kwenda Njombe, Wilaya ya Ludewa kwa ajili ya mazishi lakini
cha kushangaza nako wasanii hao waliishia nje.
Baada ya ibada kanisani, tangazo lilitolewa kwamba daftari litapita
kwa ajili ya watu wanaotaka kusafiri kwenda kuzika lakini cha
kuhuzunisha katika hilo pia walikausha ila akajitokeza mwanadada Sabrina
Rupia ‘Cath’ kwenda kumfuta machozi Mtitu.
Hatua hiyo iliwafanya wengi waone kuna tatizo kwa wasanii hao hasa wa
Bongo Muvi kwani haikuwa sahihi kumuacha mwenzao ambaye pia ni kiongozi
wa kundi hilo kwenda kumzika baba yake bila kampani.
Ikizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’ alisema:
Tulitoa ushirikiano katika kila jambo, huwezi kumlazimisha mtu kula wala kuingia kanisani. Kama kuna walionunua soda na maandazi kisha kula pale, wamekosea sana. Chakula kilikuwepo cha kutosha, kwa nini wafanye hivyo?
0 comments:
Chapisha Maoni