Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa
baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa
taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya
kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60
walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa
kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko
huo.
Mlipuko
huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako
zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi
Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo
umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia
kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi
lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa
kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini
Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili
lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo
wanayoendeleza harakati zao.
0 comments:
Chapisha Maoni