Wakulima Mkoa wa Mbeya wametakiwa kuchangamkia kilimo cha kibiashara ili waweze kubadili maisha.
Ofisa ufundi wa asasi inayojishughulisha na kilimo
cha mbogamboga na matunda ya Tanzania Horticulture Association-Taha),
Isaac Paul alitoa wito huo kwenye mafunzo maalumu ya kilimo cha kabechi
yaliyowashirikisha wakulima kutoka vikundi 12 vya Halmashauri ya Mbeya
Vijijini.
Aliwasihi wakulima wa kabechi kufuata kanuni za
kilimo bora zikiwamo za kutumia mbolea na dawa za kuua wadudu kwa wakati
ili waweze kufaidi matunda ya kazi zao.
Naye Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa kabechi
cha Simambwe, Juma Liombe alisema kikundi chake chenye wanachama 15
kimeanza kufaidika na mafunzo ya kitaalamu yanayotolewa na Taha.
Liombe alisema tatizo linalowasumbua wakulima wa kabechi ni bei ndogo. Kabechi huuzwa kati ya Sh150 na Sh200.
0 comments:
Chapisha Maoni