Kutokana na tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye kambi ya
timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha
usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo
mzima wa tukio hilo.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.TFF inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Chapisha Maoni