Alhamisi, Mei 01, 2014

JACQULINE WOLPER ATOA MSIMAMO WAKE, AFAGILIA SERIKALI 2

Jacqueline Wolper ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema yeye matakwa yake ni kuwepo kwa serikali mbili na si tatu wala ya mkataba.
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar, Wolper alisema anaamini serikali ya tatu itakuwa mzigo kwa wananchi ambao ndiyo walipa kodi.
Serikali mbili ndiyo mpango mzima, ya tatu ni mzigo, ya mkataba sioni maana yake. Halafu nataka muungano udumu, pia nitafurahi sana kama Ukawa watarudi bungeni litakapoanza tena Agosti mwaka huu
alisema Wolper.

0 comments:

Chapisha Maoni